Translate

Tangazo la Hadithi

Tuesday 21 January 2014

CHEKA UNENEPE - Mgombea Urais na Waandishi wa Habari











Jamaa mmoja ambaye alikuwa anataka kugobea nafasi ya urais chini mwake alikutana na waandishi mbalimbali kwa ajili ya kumuuliza mgombea huyo maswali. Mwandishi mmoja alianza kumuuliza swali na mazungumzo yao yalikuwa kama ifuatavyo.


Mwandishi: Muheshimiwa mgombea urais je unafikiri ni mambo gani ambayo utaweza kuifanyia nchi hii kama utashinda nafasi ya urais?


Mgombea urais: Nafikiri kitu cha kwanza nitakachofanya nikipata urais nitahakikisha natimiza ndoto yangu ya kuiwezesha nchi yangu kuwa ndio nchi ya kwanza kufika kwenye jua.


Mwandishi: Lakini muheshimiwa kwenye jua kuna joto kali sana sasa itakuwaje? si tutawapoteza hao wana sayansi utakaowatuma kwenda huko kwenye jua?


Mgombea urais: Ha ha ha haaaa Bwana mwandishi, unafikiri mimi ni mjinga? tutawatuma kwenda huko usiku  sio mchana.



Duuuuuh!!!!!!!!










No comments:

Post a Comment