Translate

Tangazo la Hadithi

Tuesday 21 January 2014

CHEKA UNENEPE - Baba na Kijana wake











Baba: Nataka umuoe msichana nitakayekuchagulia.


Kijana: Hapana baba, ninaye ninayempenda.


Baba: msichana mwenyewe niliyekuchagulia ni mtoto wa Bill Gates.


Kijana: Kama hivyo sawa.



Baba akaenda kwa Bill Gates.


Baba: Nataka binti yako aolewe na kijana wangu.


Bill Gates: Hapana!


Baba: Kijana wangu ni mkurugenzi wa Benki ya Dunia.


Bill Gates: Kama hivyo sawa.



Baba akaenda kwa rais wa benki ya dunia.


Baba: Mchague mwanangu kuwa mkurugenzi


Rais wa Benki ya Dunia: Hapana.


Baba: Ni mkwe wa Bill Gates.


Rais wa Benki ya Dunia: Kama hivyo sawa












No comments:

Post a Comment