Translate

Tangazo la Hadithi

Thursday 20 November 2014

Je Wajua?



Je Wajua kuwa mwanamuziki maarufu Shania Twain aliyeimba nyimbo kama "You're still the One", "Forever and for Always", "From this Moment On" na nyingine kibao ambaye aliolewa na mume wake aliyekuwa akiitwa Robert  Lange "Mutt" ambaye pia alikuwa Producer wake waliachana baada ya kugundulika kuwa mume huyo wa Shania Twain alikuwa akitembea na rafiki kipenzi wa Shania Twain anayeitwa Marie-Anne Thiebaud ambaye naye alikuwa ameolewa na Frederic Thiebaud raia wa Switzeland.


Shania Twain na mume wake Robert Lange ambao walioana tarehe 28 mwezi wa 12 mwaka 1993 walitengana tarehe 15 mwezi wa 5 mwaka 2008 baada ya Shania Twain kugundua uhusiano huo usiofaa kati ya mume wake na rafiki yake huyo kipenzi.


Shania Twain na mume wake Robert Lange "Mutt" waliachana kwa talaka mnamo tarehe 9 mwezi wa 6 mwaka 2010. Shania Twain na mume wake Robert Lange walijaliwa kupata mtoto mmoja wa kiume kwenye ndoa yao anayeitwa Eja aliyezaliwa mwezi wa 8 mwaka 2001.


Baada ya kuachana na mume wake Shania Twain alichumbiwa tena na Frederic Thiebaud aliyekuwa mume wa rafiki yake kipenzi Marie-Anne Thiebaud (ambaye alimchukulia mume wake) tarehe 20 mwezi wa 12 mwaka 2010 na mnamo tarehe 1 mwezi wa 1 mwaka 2011 Shania Twain na Frederic Thiebaud aliyekuwa mume wa rafiki yake kipenzi Marie-Anne Thiebaud walioana huko Rincon, Puerto Rico na mpaka sasa bado wanaendelea kuishi pamoja kama mume na mke.


Katika mahojiano aliyoyafanya na baadhi ya vyombo vya habari, Shania Twain alikiri kuumizwa sana na kitendo hicho alichofanyiwa na rafiki yake huyo kipenzi kwani alikuja kugundua kuwa rafiki yake huyo alikuwa na mahusiano na mume wake kwa zaidi ya miaka kumi na hata yeye alivyokuwa akimueleza rafiki yake huyo kuhusu matatizo ya ndoa yake na kwamba anahisi mume wake ana mwanamke mwingine rafiki yake huyo ndio alikuwa akimpa moyo kumbe hakujua kuwa yeye mwenyewe ndio anayemuharibia ndoa yake.




  • Swali la Kizushi: Je unadhani kuwa Shania Twain na Frederic Thiebaud mume wa rafiki yake Shania Twain waliamua kuoana ili kulipiza kisasi na kuwakomoa mume wa Shania Twain na rafiki yake Shania Twain au nao walipendana kweli?



Shania Twain akiwa na mume wake wa kwanza Robert Lange "Mutt"



Shania Twain (kushoto) akiwa na aliyekuwa rafiki yake kipenzi Marie-Anne Thiebaud (kulia)



Shania Twain akiwa na mume wake wa sasa Frederic Thiebaud




Shania Twain akiwa na mume wake wa sasa Frederic Thiebaud




Shania Twain akiwa na mume wake wa sasa Frederic Thiebaud




Shania Twain akiwa na mume wake wa sasa Frederic Thiebaud



Mojawapo za interviews za Shania Twain akielezea kuhusu  rafiki yake kipenzi Marie-Anne Thiebaud alivyokuwa na mahusiano na mume wake





BAADHI YA NYIMBO ZA SHANIA TWAIN ZILIZOVUMA SANA


Forever and For Always






You're Still The One 







From This Moment On