Translate

Tangazo la Hadithi

Sunday 25 August 2013

Kanisa la KKKT lachomwa moto Segerea, Dar




Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Usharika wa Segerea Dayosis ya mashariki na Pwani limechomwa moto na watu wasiojulikana usiku wa kuamkia Jumamosi ya tarehe 24.


Mchungaji wa Ushirika wa Segerea wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Mashariki na Pwani, Noah Kipingu akionyesha sehemu ya madhabahu iliyochomwa moto.

Habari za Magazetini - Leo Jumapili





























Friday 23 August 2013

KACHIKI - SEHEMU YA 3


BABA YAKE KACHIKI MZEE NYARONGO AFIKA SHULENI.





Mwalimu mkuu alimpa Kachiki Barua ili akampe baba yake mzee Nyarongo. Alipofika nyumbani alimkuta baba yake amesharudi kutoka kazini kwake anakofanya kazi ya useremala, hivyo alimkabidhi ile barua aliyopewa na mwalimu mkuu ili ampe baba yake. Alivyomkabidhi baba yake barua mama yake wa kambo alianza kumwambia baba yake Kachiki kuwa alishamueleza huyu mtoto yani Kachiki ni mkorofi na msumbufu sana, hivyo ana uhakika kabisa amefanya kosa kubwa sana na ndiyo maana walimu wameshindwa kuvumilia na safari hii wameamua kumuita aende shuleni. Inavyoonekana tayari walimu wameshachoka na vituko vyake. Baba yake Kachiki alishikwa na hasira sana na kumwambia Kachiki kuwa kama amefanya upuuzi wowote huko shuleni atamtambua. Siku hiyo Kachiki alikosa raha kabisa kwani hata yeye hakujua kwanini baba yake aliitwa shuleni. Usiku hakuweza hata kupata usingizi alikuwa akisali na kuomba Mungu amsaidie na kusiwe na tatizo kubwa aliloitiwa baba yake huko shuleni.


Asubuhi alivyoamka Kachiki aliendelea na ratiba zake za kila siku halafu akaenda shuleni. Alivyorudi kutoka shule alimkuta baba yake amesimama kwenye  mlango wa mbele wa nyumba yao, akiwa na ghadhabu huku akiwa ameshika fimbo kubwa mkononi. Mama yake wa kambo alikuwa amekaa kwenye mkeka akiwa mwenye ghadhabu pia. Kachiki hakujua kinachoendelea, alivyowakaribia aliwasalimia lakini badala ya kujibu mama yake wa kambo alianza kumgombeza kwa sauti ya juu, na baba yake hakumpa hata nafasi ya kujua nini kinachoendelea, badala yake alimshika kwa nguvu na kuanza kumpiga, alimpiga kichwani, mgongoni na sehemu zote za mwili. Wakati akimpiga hivyo mama yake wa kambo alikuwa akishirikiana naye kwa kumpa kipigo Kachiki. Maskini Kachiki hakukumbuka chochote, alichosikia kwa mara ya mwisho yalikuwa ni maneno ambayo baba yake mzee Nyarongo aliyosema “Kwanini umeitia aibu hii familia” halafu akazimia.

CHEKA UNENEPE - Polisi wa Bongo





Mazungumzo ya Polisi alipomkamata Mzungu:

Yesterday I saw you at ze maize shop {jana nilikuona dukani kwa mhindi}

When you saw me you started to six six {uliponiona ulianza kusita sita}

U ran and decided to plant a car {ulikimbia na ukaamua kupanda gari}

Now sleep down and snake well before I cut you a millet {sasa lala chini kisha nyooka vizuri kabla sijakukata mtama}

Chezea polisi wa Bongo wewe !!!





Tuesday 6 August 2013

KACHIKI - SEHEMU YA 2


WALIMU WANAJARIBU KUMSAIDIA KACHIKI





Ingawa Kachiki alikuwa na akili sana darasani alianza kushuka kwenye mitihani yake kwasababu ya matatizo aliyokuwa anayapitia. Mwanzoni alikuwa nakuwa wa kwanza darasani lakini alianza kushuka mpaka kufikia kushika nafasi ya kumi na tano kutoka mwisho kwenye darasa la wanafunzi zaidi ya hamsini.
Mwanzoni alivyokuwa anakuwa wa kwanza darasani mama yake wa kambo mama Selina alikuwa akisema kuwa anakuwa wa kwanza kwasababu anaibia kwenye mitihani, na Kachiki alipo jitahidi kujitetea mama Selina alikuja juu na kumwambia baba yake kuwa Kachiki hamuheshimu ndiyo maana anafikia hatua ya kujibizana naye. Maskini Kachiki badala ya kupongezwa kwa kufaulu akawa anaishia kuadhibiwa vikali na baba yake kwa kuchapwa viboko visivyo na idadi. 

Na alivyoanza kushuka darasani mama yake wa kambo mama Selina aliishia kufurahia na kumwambia baba yake na Kachiki kuwa mwanae alikuwa anagelezea kwenye mitihani ndio maana alikuwa anafaulu na sasa anafeli kwasababu walimu wamekuwa wakali mno na wameweka sheria kali sana kwa yeyote atakayeibia kwenye mitihani.

Siku moja mwalimu wa darasa wa Kachiki aliyekuwa anaitwa mwalimu Songambele alimwita Kachiki na kuanza kumuuliza kwanini siku zote amekuwa akichelewa kufika shuleni na pia kwanini ameanza kushuka kwenye masomo yake darasani.  Pia hata akipewa kazi za shule na mazoezi ya kwenda kufanya nyumbani amekuwa hafanyi kabisa au amekuwa hamalizi. Kachiki alianza kulia na kushindwa kujibu chochote. Mwalimu Songambele ndipo alianza kuhisi kuwa kuna kitu kinachoendelea katika maisha ya mwanafunzi wake Kachiki. Hivyo mwalimu Songambele akamuacha kwanza atulie kidogo na kunyamaza kulia ili aweze kumuuliza vizuri zaidi. Kipindi hicho Kachiki alikuwa bado ni binti mdogo akisoma darasa la nne. 

Kachiki alivyonyamaza kulia na kutulia kidogo mwalimu wake Songambele alianza kumuuliza tena, basi Kachiki alianza kumueleza kuhusu maisha yake anayoishi huko nyumbani na ratiba yake ilivyo ngumu kuanzia asubuhi anavyoamka mpaka jioni anavyorudi nyumbani kutoka shuleni na usiku anavyokwenda kulala. Na jinsi ambavyo anakosa hata muda wa kujisomea na kufanya mazoezi anayopewa shuleni. Kachiki akaendelea kumueleza mwalimu wake kuwa akifika shuleni ndio anaona sehemu yake ya kupumzikia na kupata usingizi japo kidogo. Ndio maana amekuwa mtu wa kusinzia darasani kwasababu anakuwa amechoka sana na anakuwa na usingizi mzito mno. Akiwa mlezi wa wanafunzi na pia mzazi wa watoto wake wawili wadogo mwalimu Songambele alipatwa na uchungu mno tena sana. Akapiga picha watoto wake hao wadogo ndio wawe wanaishi maisha haya! Huruma ikamjia sana. Akafikiri na kuona kuwa hata kama labda Kachiki hasemi ukweli na labda mama yake wa kambo anamfundisha tu kazi akiwa ni mtoto wa kike lakini kwa kumuangalia tu Kachiki utagundua kuwa huyu binti ana matatizo ya kifamilia na pia hana mtu wa kumuangalia na kumuongoza. Maana Kachiki alikuwa mchafu sana. Sketi yake ilikuwa imepauka na imetoboka toboka sana. Alikuwa hana viatu hivyo alikuwa akienda shuleni pekupeku. Hilo mwalimu halikumshangaza sana kwani ni wanafunzi wachache sana walikuwa wanavaa viatu shuleni hapo, wengi walikuwa wanavaa kandambili na wengine walikuwa hawana kabisa hata kandambili, lakini bado walionekana wasafi kidogo kuliko Kachiki maana hata wale wenye sare za shule zilizochakaa walikuwa wasafi kuonyesha kuwa sare zao zilikuwa zikifuliwa angalau mara kadhaa kwa wiki. Kwa karibu Kachiki alikuwa akinuka na kutoa harufu. Hata ngozi yake nzuri ya rangi ya chungwa ilikuwa imesinyaa kuonyesha kuwa hata kupata chakula kwake ni shida, ingawa uzuri wake wa sura bado ulikuwa ukionekana. Mwalimu Songambele akamuuliza Kachiki kama yeye ndio anafua nguo za watu wote pale nyumbani kwanini basi anashindwa kufua nguo zake mpaka anakuwa mchafu kiasi kile na kufikia hatua ya kutoa harufu? Kachiki akamjibu mwalimu wake wa darasa ya kuwa mama yake wa kambo mama Selina amekuwa akimwambia kuwa wakati akifua nguo zao asifue nguo zake na pia asichanganye na nguo zake kwani atawaambukiza chawa pia hamna sabuni ya kufulia nguo zake. Na pia mara nyingi akimkuta anafua nguo zake huwa anamuuliza amepata wapi sabuni na huo muda wa kupoteza mpaka kuweza kufua matambara yake badala ya kufanya kazi za pale nyumbani. Kachiki alimweleza mwalimu wake mambo mengi mno ambayo hamna mtu yeyote mwingine anayejua ingawa hata majirani walikuwa wanaona na kufahamu jinsi Kachiki alivyokuwa akiteseka lakini hawakufahamu mambo mengi ambayo Kachiki alimueleza mwalimu wake wa darasa, mwalimu Songambele.

Baada ya kusikia kuhusu maisha ya Kachiki anayoishi huko nyumbani mwalimu wa darasa akaona amshirikishe pia na mwalimu mkuu ili waone jinsi watakavyomsaidia Kachiki maana aliona hili tatizo ni kubwa sana tofauti na alivyofikiria. Akajiona yeye na walimu wenzake ni wenye makosa mno tena sana kwa kumuadhibu Kachiki kila siku kwa sababu za uchelewaji, kutohudhuria shuleni bila sababu maalum, kuja shuleni akiwa mchafu, kutofanya homework, kusinzia darasani n.k. Kama kwa siku hiyo tu amechapwa viboko karibia 15 na walimu tofauti kwa makosa tofauti na mpaka kuwa ndio mazungumzo ya walimu kwa siku hiyo  ofisini kwao. Alianza mwalimu wake wa Hisabati kusema kwamba kuna mwanafunzi anaitwa Kachiki lakini akimpa homework hafanyi na kila siku lazima amchape hata leo amemtandika sana, akadakia mwalimu wa sayansi kwa kusema kuwa yule binti ana akili lakini ni mvivu mno tena sana kama leo kaishia kumchapa viboko vya kutosha kwani aliwapa homework hajafanya pia anaishia tu kulala darasani. Akadakia mwalimu wa kingereza kwa kusema kuwa tena sijui somo lake halipendi maana kila siku yeye ana vipindi vya asubuhi viwili lakini huyo Kachiki haudhurii ama anakuja wakati kipindi kinakaribia kuisha kama leo kaingia dakika 20 kabla ya kipindi kuisha akamfukuza nje na kumwambia apige magoti juani mpaka hizo dakika 20 zitakavyoisha akitoka ndio aingie. Mwalimu wa zamu naye akadakia kama kawaida leo kamchapa viboko sita kwa kuchelewa kufika shule ingawa ni mpole lakini atakuwa na kiburi mototo gani asiyesikia kila siku anaadhibiwa lakini anarudia makosa hayo hayo. Hayo ndio mazungumzo waliyokuwa wakiyaongea walimu ofisini kwao kwa siku hiyo ambayo yakamfanya mwalimu wa darasa aamue kumuita Kachiki ili kuongea naye. Akiwa mwalimu wa darasa hata yeye mwalimu Songambele amekuwa akimuadhibu sana Kachiki kwa kudhani kuwa labda ni mvivu hivyo kwa kuadhibiwa atajirekebisha, baada ya kumsikiliza Kachiki akajikuta akinyong’onyea na kujilaumu kwa kiasi fulani kushindwa kulitambua hilo mapema.  

Hivyo baada ya mashauriano ya hapa na pale mwalimu mkuu na mwalimu wa darasa waliamua kumuita mzazi wa Kachiki, baba yake mzee Nyarongo kufika shuleni kwasababu walifikiri ya kuwa itakuwa baba yake hafahamu kinachomtokea binti yake nyumbani. Maana imekuwa ni tabia ya mama wengi wa kambo kuwa wanafiki na kuonyesha upendo kwa watoto wao wa kambo pindi baba zao wawapo nyumbani lakini wakiondoka tu ndio mama wa kambo wanapobadilika na mateso kwa watoto hao kuanza.