Translate

Tangazo la Hadithi

Tuesday 28 April 2015

Ujumbe wa Leo



Cheka na watu wote, ishi vizuri na watu wote yaani majirani, marafiki, ndugu na jamaa, lakini kuwa makini sana na usiamini sana watu kupita kiasi. Kwani watu unaowachekea na kuwapenda usidhani na wao wanakuchekea na kukupenda mioyoni mwao. Hivyo CHUKUA TAHADHARI KABLA YA HATARI!





Songa Mbele - Bahati Bukuku



Friday 10 April 2015

Je Wajua?








Je Wajua kwamba muigizaji na producer Michael Douglas na mke wake Catherine Zeta - Jones ambaye naye pia ni muigizaji wamezaliwa tarehe moja na mwezi mmoja ingawa miaka tofauti.


Michael Douglas amezaliwa tarehe 25 mwezi wa 9 mwaka 1944 na mke wake Catherine Zeta - Jones yeye amezaliwa tarehe 25 mwezi wa 9 mwaka 1969. Wote wawili wamezaliwa tarehe 25 na pia wamepishana miaka 25.


Michael Douglas na mke wake Catherine Zeta - Jones wamejaliwa kupata watoto wawili, wa kiume mmoja na wa kike mmoja.



Je kuna couple yoyote unayoijua ambayo husherehekea siku moja ya kuzaliwa yaani ambao wamezaliwa tarehe moja na mwezi mmoja hata kama miaka ni tofauti?