Translate

Tangazo la Hadithi

Tuesday 7 January 2014

CHEKA UNENEPE - Juma kwenye sherehe ya wanyakyusa






Jamaa mmoja aitwaye JUMA alivamia sherehe ya harusi ya Wanyakyusa na kujifanya na yeye ni mwanafamilia wa bwana harusi. Wakati wa utambulisho wa ndugu wa bwana harusi wakaanza kusimama mmoja mmoja na kutaja jina lake.

Wa kwanza akasema: Naitwa Mwakalebela.

Wa pili akasema: Naitwa Mwasikili

Wa tatu akasema: Naitwa Mwakipesile 

Wa nne akasema: Naitwa Mwakasungura

Wa tano akasema: Naitwa Mwambela

Wa sita akasema: Naitwa Mwakatundu

Ilipofika zamu ya Juma akafikiria kisha akadhani kuwa kila jina katika kabila lile ni lazima uanze na "MWA", basi akainuka kwa makonfidensi na kupaza sauti "Naitwa MWAJUMA"








No comments:

Post a Comment