Translate

Tangazo la Hadithi

Sunday 9 February 2014

Wajue wake wa Rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini






Rais Jacob Zuma akiwa na wake zake wanne; kutoka kushoto ni Bongi Ngema, Nompumelelo Ntuli, Rais Jacob Zuma, Thobeka Madiba Zuma na  Getrude Sizakele Khumalo kwenye sherehe ya Rais Jacob Zuma kutimiza miaka 70





Rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini ameoa mara sita, mpaka sasa anaishi na wake zake wanne baada ya kuachana na mke wake mmoja na mwingine kufariki dunia.






Wake wa Rais Jacob Zuma, kutoka kushoto ni Nompumelelo Ntuli, Thobeka Madiba Zuma na Bongi Ngema






1. Getrude Sizakele Khumalo



Getrude Sizakele Khumalo ni mke wa kwanza wa Rais Jacob Zuma. Rais Jacob Zuma alimuoa mke wake wa kwanza Getrude Sizakele Khumalo mnamo mwaka 1973. Rais Jacob Zuma na mke wake wa Kwanza Getrude hawajabahatika kupata mtoto.





Rais Jacob Zuma akiwa na mke wake wa kwanza Getrude Sizakele Khumalo




2. Kate Mantsho



Rais Jacob Zuma alimuoa mke wake wa pili Kate Mantsho ambaye alikuwa ni raia wa Msumbiji mnamo mwaka 1976. Kate Mantsho alifariki mnamo mwaka 2000 kwa kujiua.






3. Nkosazana Dlamini - Zuma



Rais Jacob Zuma alimuoa mke wake wa tatu Nkosazana Dlamini - Zuma mnamo mwaka 1982, Rais Jacob Zuma na mke wake Nkosazana Dlamini - Zuma waliachana mwaka 1998.












4. Nompumelelo Ntuli




Rais Jacob Zuma alimuoa mke wake wa nne Nompumelelo Ntuli mnamo mwaka 2008.




Rais Jacob Zuma akiwa na mke wake wa nne Nompumelelo Ntuli






5. Thobeka Stacy Mabhija ambaye pia anajulikana kama Thobeka Madiba Zuma




Rais Jacob Zuma alimuoa mke wake wa Tano Thobeka Madiba Zuma mnamo mwaka 2010.





Rais Jacob Zuma akiwa na mke wake wa tano Thobeka Madiba Zuma kwenye sherehe ya kusherehekea miaka 40 ya tangu kuzaliwa mke wake huyo






6. Gloria Bongekile Ngema ambaye pia anajulikana kama Bongi Ngema




Rais Jacob Zuma alimuoa mke wake wa sita Bongi Ngema mwaka 2012.




Rais Jacob Zuma akiwa na mke wake wa sita Bongi Ngema





No comments:

Post a Comment