Translate

Tangazo la Hadithi

Thursday, 25 July 2013

Ajali ya treni Spain


Watu kadhaa wamefariki na wengine kujeruhiwa baada ya kutokea kwa ajali ya treni huko Spain siku ya Jumatano tarehe 24 July. Inasadikiwa kuwa zaidi ya watu 70 wamefariki dunia na wengine zaidi ya 130 wamejeruhiwa. 


Shughuli za uokoaji zikiendelea


Maiti kutoka kwenye treni iliyopata ajali wakihifadhiwa na majeruhi wakipewa huduma ya kwanza


Watu wakiokolewa kutoka kwenye treni iliyopata ajali






Hatimaye mke wa Prince William, Kate Middleton ajifungua mtoto wa kiume









Hatimaye mjukuu wa Malkia Elizabeth wa Uingereza Prince William apata mtoto baada ya mke wake Kate Middleton kujifungua mtoto wa kiume mwenye uzito wa kilo 3.79 siku ya Jumatatu tarehe 22 July, 2013 katika hospitali ya St. Mary's iliyoko Magharibi mwa London. Tayari mtoto huyo wa kifalme ameshapewa jina la George Alexander Louis. 




Mtoto wa Prince William na Kate Middleton






Mtoto wa Prince William na Kate Middleton






Prince William akiwa na mke wake Kate Middleton na mtoto wao






Prince William akiwa na mke wake Kate Middleton na mtoto wao







Prince William na mke wake Kate Middleton wakitoka hospitali






Kate Middleton akiwa amembeba mwanae Prince George






Waingereza wakishangilia baada ya kupata taarifa za kuzaliwa mtoto wa Prince William ambaye ni mjukuu wa malkia Elizabeth wa Uingereza.




Wednesday, 17 July 2013

CHEKA UNENEPE - Bwana John








John alionekana kupona hivyo akatolewa kwenye hospitali ya machizi arudishwe kwao.

Asubuhi moja akachukuliwa akapelekwa hadi jirani na kwake akaulizwa unapafahamu hapa?


John: ndiyo, nyumba yangu ilee! Ghafla mlango wa nyumba ile ukafunguka wakatoka watoto wawili wamevaa sare za shule,

John: hee watoto wangu wale wanaenda shule

mara akatoka mwanamke, John akafurahi, mke wangu yule jamani mke wangu.

madaktari walianza kumfungulia John atoke kwenye gari! Mara akatoka mwanaume kwenye ile nyumba, John akaangalia kwa makini kisha akaruka kwa furaha

John: Mimi yule naenda kazini unaona nilivyopendeza na ile suti ya mariedo niliyonunua Somalia.











Sunday, 7 July 2013

Rubani wa ndege ya Korea Kusini Asiana Airlines iliyoanguka San Francisco alikuwa mafunzoni

Ndege ya South Korea Asiana Airlines iliyoanguka jumamosi ya tarehe 6 July 2013

Msemaji wa Asiana Airlines ndege ya Korea ya kusini iliyo anguka jumamosi ya tarehe 6 July wakati inatua kwenye uwanja wa kimataifa wa San Francisco amesema ya kuwa rubani aliyekuwa anahusika na utuaji wa ndege hiyo alikuwa mafunzoni.

Msemaje huyo amefafanua kuwa Rubani huyo mwenye jina la Lee Kang-Kook alianza kazi Asiana Airlines kama intern (mwanafunzi wa mafunzo ya vitendo) mnamo mwaka 1994, na ana ujuzi wa masaa 9,793 katika urushaji wa ndege, lakini ana ujuzi wa masaa 43 tu wa kurusha ndege za Boeing 777.

Msemaji huyo amefafanua pia kuwa Lee Kang-Kook ana ujuzi wa kutosha na ameshawahi kurusha ndege za aina mbalimbali kama B747 kwenda San Francisco. Lee Kang-Kook alikuwa anasaidiana na Rubani  mwenzake Lee Jeong-min ambaye ana ujuzi zaidi wa kurusha ndege za Boeing 777 kwa masaa 3,220 na ujuzi wa jumla ya masaa 12,387 ya kurusha ndege, hivyo bado chanzo hasa cha ajali hakijafahamika kama ni matatizo ya kiufundi ama ni tatizo la rubani.

Source:Reuters

Ndege ya Korea Kusini Asiana Airlines yapata ajali Marekani




Watu 2 wamefariki dunia na wengine kadhaa kujeruhiwa baada ya ndege ya Korea Kusini Asiana Airlines kushindwa kutua kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa San Francisco Nchini Marekani siku ya jumamosi tarehe 6, July.

Thursday, 4 July 2013

Mke wa Rais mstaafu wa Afrika kusini Bibi Graca Machel azungumzia afya ya mumewe



Mke wa rais mstaafu wa Africa Kusini bibi Graca Machel azungumzia afya ya mumewe bwana Nelson Mandela. Akizungumza katika shughuli ya kumpa tunzo ya heshima rais mstaafu huyo ambaye kwa sasa ni mgonjwa hospitalini bibi Graca Machel amesema kuwa ingawa bwana Mandela anaumwa lakini hayupo kwenye maumivu makali sana. Kauli ambayo kwa kiasi fulani inapingana na madaktari wanaomtibu bwana Mandela ambapo inasemekana wameishauri familia ya bwana Mandela kutoa idhini ya kuizima mashine inayomsaidia kupumulia.





Ujumbe mbalimbali wa kumtakia bwana Nelson Mandela apone haraka ukiwa umewekwa nje ya nyumba yake huko Johannesburg, South Africa.


Monday, 1 July 2013

Rais Barack Obama awasili Tanzania na kupokelewa kwa shangwe






Rais Barack Obama amewasili leo nchini Tanzania na kupokewa kwa shangwe na Watanzania. Rais Barack Obama amefika Tanzania akitokea South Africa alikokuwa kwa ziara ya siku mbili. Rais Barack Obama ameambatana pia na familia yake akiwepo mke wake Michelle Obama na watoto wao Malia na Sasha Obama. Akiwa uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere Rais Barack Obama alilakiwa na mwenyeji wake Rais Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe mama Salma Kikwete na viongozi mbalimbali.



Rais Barack Obama akiongozwa na mwenyeji wake Rais wa Tanzania muheshimiwa Rais Jakaya Mrisho Kikwete.


Rais Barack Obama na mke wake Michelle Obama wakipokea maua kutoka kwa watoto mara baada ya kufika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.



Rais Barack Obama akicheza ngoma ya utamaduni mara alipowasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere Dar es salaam, Tanzania.


 Rais Barack Obama na mkewe Michell Obama pamoja na wenyeji wao Rais Kikwete na mkewe mama Salma Kikwete wakisalimiana na wananchi waliokuja kumlaki katika Ikulu ya Dar es salaam.



Rais Barack Obama na Rais Kikwete wakihutubia waandishi wa habari Ikulu Dar es salaam.





Rais Obama akisalimiana na wananchi mbalimbali waliokuja kumlaki Ikulu ya Dar es salaam

Rais Obama akiwa ameongozana na mkuu wa majeshi ya Tanzania Meja Jenerali Davis Mwamunyange.





Kinamama wakiwa wamevaa kanga zenye sura ya Obama


 Akikagua gwaride la heshima


 Barack Obama Drive, mandhari ya kupendeza kabisa. Naona mbu wote wamehama kwa muda.



Michelle Obama atembelea ofisi za WAMA Foundation Leo





Mke wa Rais wa Marekani Michelle Obama ametembelea ofisi za Foundation ya WAMA inayosimamiwa na mama Kikwete leo Jumatatu ya tarehe. Akiwa katika ofisi za WAMA Michelle Obama alikutana na mama Salma Kikwete na wake wa viongozi mbalimbali wa Tanzania.


                                   
Mke wa rais wa Marekani, Michelle Obama akisalimiana kwa furaha na mke wa rais wa Tanzania mama Salma Kikwete alipowasili kwenye ofisi za WAMA Dar es salaam.


Michelle Obama akiwasili katika ofisi za WAMA, Dar es salaam Tanzania

Wake wa viongozi mbalimbali wakimlaki mke wa rais wa Marekani Michelle Obama alipotembelea ofisi za WAMA leo