Translate

Tangazo la Hadithi

Showing posts with label Marekani. Show all posts
Showing posts with label Marekani. Show all posts

Monday, 1 July 2013

Michelle Obama atembelea ofisi za WAMA Foundation Leo





Mke wa Rais wa Marekani Michelle Obama ametembelea ofisi za Foundation ya WAMA inayosimamiwa na mama Kikwete leo Jumatatu ya tarehe. Akiwa katika ofisi za WAMA Michelle Obama alikutana na mama Salma Kikwete na wake wa viongozi mbalimbali wa Tanzania.


                                   
Mke wa rais wa Marekani, Michelle Obama akisalimiana kwa furaha na mke wa rais wa Tanzania mama Salma Kikwete alipowasili kwenye ofisi za WAMA Dar es salaam.


Michelle Obama akiwasili katika ofisi za WAMA, Dar es salaam Tanzania

Wake wa viongozi mbalimbali wakimlaki mke wa rais wa Marekani Michelle Obama alipotembelea ofisi za WAMA leo


Saturday, 29 June 2013

Rais Jakaya Kikwete na watanzania wajiandaa kumpokea Rais Obama wa USA



Rais Kikwete na Rais Obama wakiwa Ikulu ya Marekani, Washington DC, 2009


Rais Jakaya Mrisho Kikwete na watanzania wamejiandaa kumpokea Rais Barack Obama wa Marekani ambaye anatokea South Africa alikokuwa kwa ziar ya siku 2. Akiwa South Africa Rais Obama amekutana na familia ya Mandela. Rais Obama pia atatembelea kisiwa cha Robben ambako alifungwa Rais mstaafu wa Afrika ya Kusini Mzee Nelson Mandela kwa miaka 18 kati ya miaka 27 aliyokaa jela.
Rais Obama pia atatembelea community centre pamoja na Askofu Desmond Tutu wa Afrika Kusini ambaye pia ni rafiki mkubwa wa rais mstaafu mzee Nelson Mandela.
Rais Obama atawasili nchini Tanzania siku ya Jumatatu tarehe moja ambapo ndiyo itakuwa nchi yake ya mwisho kutembelea kwenye ziara yake hii ya Afrika.