Translate

Tangazo la Hadithi

Showing posts with label vichekesho.. Show all posts
Showing posts with label vichekesho.. Show all posts

Friday, 23 August 2013

CHEKA UNENEPE - Polisi wa Bongo





Mazungumzo ya Polisi alipomkamata Mzungu:

Yesterday I saw you at ze maize shop {jana nilikuona dukani kwa mhindi}

When you saw me you started to six six {uliponiona ulianza kusita sita}

U ran and decided to plant a car {ulikimbia na ukaamua kupanda gari}

Now sleep down and snake well before I cut you a millet {sasa lala chini kisha nyooka vizuri kabla sijakukata mtama}

Chezea polisi wa Bongo wewe !!!





Wednesday, 17 July 2013

CHEKA UNENEPE - Bwana John








John alionekana kupona hivyo akatolewa kwenye hospitali ya machizi arudishwe kwao.

Asubuhi moja akachukuliwa akapelekwa hadi jirani na kwake akaulizwa unapafahamu hapa?


John: ndiyo, nyumba yangu ilee! Ghafla mlango wa nyumba ile ukafunguka wakatoka watoto wawili wamevaa sare za shule,

John: hee watoto wangu wale wanaenda shule

mara akatoka mwanamke, John akafurahi, mke wangu yule jamani mke wangu.

madaktari walianza kumfungulia John atoke kwenye gari! Mara akatoka mwanaume kwenye ile nyumba, John akaangalia kwa makini kisha akaruka kwa furaha

John: Mimi yule naenda kazini unaona nilivyopendeza na ile suti ya mariedo niliyonunua Somalia.