Ndege ya South Korea Asiana Airlines iliyoanguka jumamosi ya tarehe 6 July 2013
Msemaji wa Asiana Airlines ndege ya Korea ya kusini iliyo anguka jumamosi ya tarehe 6 July wakati inatua kwenye uwanja wa kimataifa wa San Francisco amesema ya kuwa rubani aliyekuwa anahusika na utuaji wa ndege hiyo alikuwa mafunzoni.
Msemaje huyo amefafanua kuwa Rubani huyo mwenye jina la Lee Kang-Kook alianza kazi Asiana Airlines kama intern (mwanafunzi wa mafunzo ya vitendo) mnamo mwaka 1994, na ana ujuzi wa masaa 9,793 katika urushaji wa ndege, lakini ana ujuzi wa masaa 43 tu wa kurusha ndege za Boeing 777.
Msemaji huyo amefafanua pia kuwa Lee Kang-Kook ana ujuzi wa kutosha na ameshawahi kurusha ndege za aina mbalimbali kama B747 kwenda San Francisco. Lee Kang-Kook alikuwa anasaidiana na Rubani mwenzake Lee Jeong-min ambaye ana ujuzi zaidi wa kurusha ndege za Boeing 777 kwa masaa 3,220 na ujuzi wa jumla ya masaa 12,387 ya kurusha ndege, hivyo bado chanzo hasa cha ajali hakijafahamika kama ni matatizo ya kiufundi ama ni tatizo la rubani.
Source:Reuters
No comments:
Post a Comment