Translate

Tangazo la Hadithi

Showing posts with label Hadithi ya Jasmine. Show all posts
Showing posts with label Hadithi ya Jasmine. Show all posts

Wednesday, 22 March 2023

Hadithi ya Kachiki

Sikiliza Hadithi ya Kachiki hapa 👇






Kachiki ni hadithi inayomuhusu binti wa kiafrika ambaye amekulia kwenye mazingira ya kiafrika na kupitia vikwazo vingi katika maisha yake. Je atafanikiwa kuviruka vikwazo na viunzi vilivyopo mbele ya maisha yake? Je ni vikwazo vipi hivyo?


Jiandae kusikiliza Hadithi hii ya kusisimua ambayo itakufundisha na kukuburudisha. 



Tuesday, 18 March 2014

JASMINE - SEHEMU YA 2








Helena aliendelea kuwalea Jasmine na Vicky kwa tabu mpaka Jasmine alivyomaliza darasa la saba. Baada ya Jasmine kumaliza darasa la saba matokeo yalivyotoka Jasmine alikuwa ni miongoni mwa wanafunzi waliofaulu na kuchaguliwa kwenda kusoma shule ya serikali. Hivyo kufaulu kwa Jasmine kulimsaidia kidogo mama yake mdogo maana hela zilizokuwa zinahitajika hazikuwa nyingi sana kama kwenye shule za binafsi. Kila jioni baada ya kutoka shuleni Jasmine alimsaidia mama yake mdogo kuuza kwenye biashara zake.

Wakati Jasmine akianza form one huku akiwa na miaka 15 Vicky naye alikuwa darasa la 3 huku akiwa na miaka 10, hivyo wakati mwingi wakiwa nyumbani baada ya kumaliza kumsaidia mama yao Helena kuuza kwenye biashara zake za chakula Jasmine alikuwa akimfundisha Vicky hasa somo la hesabu.

Miaka ikaenda na kukatika hatimaye Jasmine alimaliza form four akiwa na miaka 18 na wakati huo Vicky naye alikuwa na miaka 13 akisoma darasa la sita.  Majibu ya kina Jasmine ya form four yalivyotoka matokeo yake hayakuwa mazuri alikuwa amepata daraja la nne. Kwa kipato cha mama yake mdogo Helena ilikuwa sio rahisi tena kumuendeleza hivyo ndio ikawa mwisho wa Jasmine kuendelea na shule. Hivyo muda wake mwingi akawa anautumia kumsaidia mama yake mdogo Helena kwenye biashara zake za kupika chakula.




USIKOSE KUSOMA HADITHI HII YA JASMINE SEHEMU YA 3…




JASMINE - SEHEMU YA 1







Jasmine ni binti yatima ambaye alifiwa na wazazi wake akiwa bado mdogo. Baba yake aliyekuwa anaitwa mzee Jumbe alifariki wakati Jasmine akiwa na umri wa miaka 3 tu hivyo akalelewa na mama yake ambaye naye alifariki wakati Jasmine akiwa na umri wa miaka 10 na akisoma darasa la tatu, hivyo jukumu la kumlea Jasmine aliachiwa mama yake mdogo aliyeitwa Helena. Jasmine alianza kuishi na mama yake mdogo Helena mara tu alipofiwa na mama yake mzazi.

Helena mama yake mdogo na Jasmine naye pia alikuwa na binti aliyeitwa Vicky ambaye alikuwa mdogo kwa Jasmine kwa miaka mitano. Wakati Jasmine alivyokuja kuanza kuishi na mama yake mdogo Vicky alikuwa anasoma chekechea na alikuwa na miaka 5. Baba yake na Vicky alimkataa Helena wakati akiwa tu na mimba ya Vicky. Hivyo Vicky mpaka anafikisha umri huo wa miaka mitano hakuwahi kumjua wala kumuona baba yake mzazi. Baada ya kukataliwa na baba yake Vicky tangu akiwa na mimba Helena aliamua tu kumlea mwenyewe binti yake Vicky huku akiendelea kujishughulisha na biashara ndogo ndogo.

Dada yake Helena mama Jasmine alivyofariki Helena aliamua pia kuchukua jukumu la kumlea mtoto wa marehemu dada yake. Kipato cha Helena hakikuwa kikubwa kwani alikuwa anajishughulisha na biashara ndogo ndogo za kuuza chakula na vitafunio kama chapati na vitumbua  lakini alijitahidi kuhakikisha watoto wake Jasmine na Vicky wanapata angalau milo 2 hata mi 3 kwa siku.

Helena alimpenda sana Jasmine kama mtoto wake wa kumzaa. Kila akikaa na kumuangalia Jasmine alikuwa akipatwa na huzuni sana na alimkumbuka sana marehemu dada yake na jinsi walivyokuwa pamoja na michezo yote waliyokuwa wakicheza mpaka walivyokuwa wakubwa. Hivyo alijitahidi kila awezavyo ili Jasmine na Vicky wawe na furaha. Pia alijitahidi Jasmine na Vicky wasome ili waje kuwa na elimu itakayokuja kuwasaidia kwenye maisha yao ya baadaye. Yeye na dada yake mama Jasmine hawakusoma sana waliishia tu darasa la saba kwa sababu wazazi wao hawakuwa na uwezo wa kuwaendeleza kielimu. Dada yake mama Jasmine alivyomaliza tu darasa la saba alikaa nyumbani na alivyo pata mchumba ambaye ndiye baba yake na Jasmine akaolewa na kumchukua na yeye Heelena na kuanza kuishi wote mpaka pale Helena alivyoamua kuanza kujitegemea mwenyewe akampa mtaji kidogo wa kuanzisha hiyo biashara yake ya kupika chakula na vitafunio kutoka kwenye ki akiba kidogo alichokuwa nacho.

Baada ya kuolewa na mzee Jumbe mama yake na Jasmine aliishi kwenye mateso ya hali ya juu, mume wake mzee Jumbe alikuwa akimpiga na kumnyanyasa sana, pia alikuwa ni mlevi wa kupindukia. Baada ya mzee Jumbe kufariki dunia wakati Jasmine akiwa na miaka 3 tu mama Jasmine aliamua kutoolewa tena ili amtunze mwanae kwanza huku akifanya biashara ndogondogo lakini bahati mbaya naye alifariki wakati mwanae Jasmine akiwa na umri wa miaka 10. Helena alijitahidi sana Jasmine na Vicky wasome ili wasije kuishi kama wao. Aliamini kuwa labda yeye na dada yake wangesoma kidogo labda wangepata kazi ambazo zingewasaidia kujikwamua na maisha. Ingawa Helena alikuwa anawalea na kuwasomesha kwa taabu kina Jasmine na Vicky lakini alijitahidi sana watoto wake hao wasikose chakula, alihakikisha pia kabla hawajaenda shule wamekunywa chai au uji na kuwafungia chapati au vitumbua alivyokuwa akipika vya kwenda navyo shule.





USIKOSE KUSOMA HADITHI HII YA JASMINE SEHEMU YA 2…


Friday, 14 March 2014

Jasmine...














Je Jasmine atakuwa amepatwa na kufikwa na nini?


Usikose kusoma Hadithi hii nyingine ya kusisimua ya Jasmine ambayo itakuelimisha na kukuburudisha pia hivi karibuni hapa hapa kwenye blog ya Habari na Hadithi Zetu.