Jasmine
ni binti yatima ambaye alifiwa na wazazi wake akiwa bado mdogo. Baba yake
aliyekuwa anaitwa mzee Jumbe alifariki wakati Jasmine akiwa na umri wa miaka 3
tu hivyo akalelewa na mama yake ambaye naye alifariki wakati Jasmine akiwa na
umri wa miaka 10 na akisoma darasa la tatu, hivyo jukumu la kumlea Jasmine
aliachiwa mama yake mdogo aliyeitwa Helena. Jasmine alianza kuishi na mama yake
mdogo Helena mara tu alipofiwa na mama yake mzazi.
Helena
mama yake mdogo na Jasmine naye pia alikuwa na binti aliyeitwa Vicky ambaye
alikuwa mdogo kwa Jasmine kwa miaka mitano. Wakati Jasmine alivyokuja kuanza
kuishi na mama yake mdogo Vicky alikuwa anasoma chekechea na alikuwa na miaka
5. Baba yake na Vicky alimkataa Helena wakati akiwa tu na mimba ya Vicky. Hivyo
Vicky mpaka anafikisha umri huo wa miaka mitano hakuwahi kumjua wala kumuona
baba yake mzazi. Baada ya kukataliwa na baba yake Vicky tangu akiwa na mimba
Helena aliamua tu kumlea mwenyewe binti yake Vicky huku akiendelea
kujishughulisha na biashara ndogo ndogo.
Dada
yake Helena mama Jasmine alivyofariki Helena aliamua pia kuchukua jukumu la
kumlea mtoto wa marehemu dada yake. Kipato cha Helena hakikuwa kikubwa kwani
alikuwa anajishughulisha na biashara ndogo ndogo za kuuza chakula na vitafunio
kama chapati na vitumbua lakini
alijitahidi kuhakikisha watoto wake Jasmine na Vicky wanapata angalau milo 2
hata mi 3 kwa siku.
Helena
alimpenda sana Jasmine kama mtoto wake wa kumzaa. Kila akikaa na kumuangalia
Jasmine alikuwa akipatwa na huzuni sana na alimkumbuka sana marehemu dada yake
na jinsi walivyokuwa pamoja na michezo yote waliyokuwa wakicheza mpaka
walivyokuwa wakubwa. Hivyo alijitahidi kila awezavyo ili Jasmine na Vicky wawe
na furaha. Pia alijitahidi Jasmine na Vicky wasome ili waje kuwa na elimu
itakayokuja kuwasaidia kwenye maisha yao ya baadaye. Yeye na dada yake mama
Jasmine hawakusoma sana waliishia tu darasa la saba kwa sababu wazazi wao
hawakuwa na uwezo wa kuwaendeleza kielimu. Dada yake mama Jasmine alivyomaliza
tu darasa la saba alikaa nyumbani na alivyo pata mchumba ambaye ndiye baba yake
na Jasmine akaolewa na kumchukua na yeye Heelena na kuanza kuishi wote mpaka
pale Helena alivyoamua kuanza kujitegemea mwenyewe akampa mtaji kidogo wa
kuanzisha hiyo biashara yake ya kupika chakula na vitafunio kutoka kwenye ki
akiba kidogo alichokuwa nacho.
Baada
ya kuolewa na mzee Jumbe mama yake na Jasmine aliishi kwenye mateso ya hali ya
juu, mume wake mzee Jumbe alikuwa akimpiga na kumnyanyasa sana, pia alikuwa ni
mlevi wa kupindukia. Baada ya mzee Jumbe kufariki dunia wakati Jasmine akiwa na
miaka 3 tu mama Jasmine aliamua kutoolewa tena ili amtunze mwanae kwanza huku
akifanya biashara ndogondogo lakini bahati mbaya naye alifariki wakati mwanae
Jasmine akiwa na umri wa miaka 10. Helena alijitahidi sana Jasmine na Vicky
wasome ili wasije kuishi kama wao. Aliamini kuwa labda yeye na dada yake
wangesoma kidogo labda wangepata kazi ambazo zingewasaidia kujikwamua na
maisha. Ingawa Helena alikuwa anawalea na kuwasomesha kwa taabu kina Jasmine na
Vicky lakini alijitahidi sana watoto wake hao wasikose chakula, alihakikisha
pia kabla hawajaenda shule wamekunywa chai au uji na kuwafungia chapati au
vitumbua alivyokuwa akipika vya kwenda navyo shule.
USIKOSE KUSOMA HADITHI HII
YA JASMINE SEHEMU YA 2…
No comments:
Post a Comment