Helena
aliendelea kuwalea Jasmine na Vicky kwa tabu mpaka Jasmine alivyomaliza darasa
la saba. Baada ya Jasmine kumaliza darasa la saba matokeo yalivyotoka Jasmine
alikuwa ni miongoni mwa wanafunzi waliofaulu na kuchaguliwa kwenda kusoma shule
ya serikali. Hivyo kufaulu kwa Jasmine kulimsaidia kidogo mama yake mdogo maana
hela zilizokuwa zinahitajika hazikuwa nyingi sana kama kwenye shule za binafsi.
Kila jioni baada ya kutoka shuleni Jasmine alimsaidia mama yake mdogo kuuza
kwenye biashara zake.
Wakati
Jasmine akianza form one huku akiwa na miaka 15 Vicky naye alikuwa darasa la 3
huku akiwa na miaka 10, hivyo wakati mwingi wakiwa nyumbani baada ya kumaliza
kumsaidia mama yao Helena kuuza kwenye biashara zake za chakula Jasmine alikuwa
akimfundisha Vicky hasa somo la hesabu.
Miaka
ikaenda na kukatika hatimaye Jasmine alimaliza form four akiwa na miaka 18 na
wakati huo Vicky naye alikuwa na miaka 13 akisoma darasa la sita. Majibu ya kina Jasmine ya form four
yalivyotoka matokeo yake hayakuwa mazuri alikuwa amepata daraja la nne. Kwa
kipato cha mama yake mdogo Helena ilikuwa sio rahisi tena kumuendeleza hivyo
ndio ikawa mwisho wa Jasmine kuendelea na shule. Hivyo muda wake mwingi akawa
anautumia kumsaidia mama yake mdogo Helena kwenye biashara zake za kupika
chakula.
USIKOSE KUSOMA HADITHI HII
YA JASMINE SEHEMU YA 3…
No comments:
Post a Comment