Aliyekuwa Katibu mkuu wa Chadema, Zitto Kabwe ameshinda kesi aliyoifungua mahakamani dhidi ya chama hicho. Zitto ambaye ni mbunge wa Kigoma Kaskazini, aliiomba Mahakama Kuu, Kanda ya Dar es salaam kuizuia Kamati Kuu (CC) ya Chadema kumjadili au kuchukua uamuzi wowote kuhusu uanachama wake hadi kesi yake ya msingi itakaposikilizwa na kutolewa uamuzi.
Mahakama kuu jana tarehe 7 January 2014 ilikubaliana na maombi na hoja za Zitto na kutoa zuio kwa Kamati Kuu ya Chadema au chombo chake chochote cha uamuzi kumjadili na kutoa uamuzi wowote kuhusiana na uanachama wake, hadi kesi yake ya msingi itakaposikilizwa na kuamuliwa.
Zitto alikuwa akitetewa na wakili wake Albert Msando na Chama cha Chadema walikuwa wakitetewa na Mawakili Tundu Lissu na Peter Kibatala.
Muheshimiwa Zitto Kabwe pamoja na wakili wake Albert Msando (kulia) walivyokuwa wakiwasili mahakamani kusikiliza kesi yake
Wakili wa chama cha Chadema Muheshimiwa Tundu Lisu akizungumza na vyombo vya habari nje ya mahakama kuu ya Dar es salaam juu ya maamuzi yaliyotolewa na mahakama hiyo kuhusiana na kesi ya Zito Kabwe dhidi ya chama cha Chadema.
Zitto Kabwe akipewa mkono na wakili wa Chadema, Tundu Lisu baada ya kushinda kesi yake
WAFUASI WA CHADEMA NAO WAKIWA NA MABANGO
No comments:
Post a Comment