Translate

Tangazo la Hadithi

Showing posts with label Zitto Kabwe. Show all posts
Showing posts with label Zitto Kabwe. Show all posts

Wednesday, 8 January 2014

ZITTO KABWE ASHINDA KESI DHIDI YA CHADEMA






Aliyekuwa Katibu mkuu wa Chadema, Zitto Kabwe ameshinda kesi aliyoifungua mahakamani dhidi ya chama hicho. Zitto ambaye ni mbunge wa Kigoma Kaskazini, aliiomba Mahakama Kuu, Kanda ya Dar es salaam kuizuia Kamati Kuu (CC) ya Chadema kumjadili au kuchukua uamuzi wowote kuhusu uanachama wake hadi kesi yake ya msingi itakaposikilizwa na kutolewa uamuzi. 

Mahakama kuu jana tarehe 7 January 2014 ilikubaliana na maombi na hoja za Zitto na kutoa zuio kwa Kamati Kuu ya Chadema au chombo chake chochote cha uamuzi kumjadili na kutoa uamuzi wowote kuhusiana na uanachama wake, hadi kesi yake ya msingi itakaposikilizwa na kuamuliwa.

Zitto alikuwa akitetewa na wakili wake Albert Msando na Chama cha Chadema walikuwa wakitetewa na Mawakili Tundu Lissu na Peter Kibatala.



Muheshimiwa Zitto Kabwe pamoja na wakili wake Albert Msando (kulia) walivyokuwa wakiwasili mahakamani kusikiliza kesi yake 





Wakili wa chama cha Chadema Muheshimiwa Tundu Lisu akizungumza na vyombo vya habari nje ya mahakama kuu ya Dar es salaam juu ya maamuzi yaliyotolewa na mahakama hiyo kuhusiana na kesi ya Zito Kabwe dhidi ya chama cha Chadema.





Zitto Kabwe akipewa mkono na wakili wa Chadema, Tundu Lisu baada ya kushinda kesi yake




WAFUASI WA CHADEMA NAO WAKIWA NA MABANGO









Tuesday, 7 January 2014

Viongozi wetu - Wabunge na viongozi mbalimbali walivyokuwa kwenye mafunzo ya muda mfupi ya jeshi la kujenga Taifa (JKT), March 2013



Kutoka Kushoto mstari wa mbele ni Mbunge wa Kawe Halima Mdee (Chadema) na Mbunge wa viti maalum CCM, Ester Bulaya





Kutoka kushoto mstari wa mbele ni Mbunge wa Kinondoni Idd Azzan na anayefuatia ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini Zitto Kabwe





















Wakiwa shambani pamoja ni wabunge Zitto Kabwe, Iddi Azzan, Abdallah Haji, Raya Ibrahim na Anthony Mbassa.





Kutoka Kushoto waliokaa ni mbunge Neema Hamid, Ester Bulaya na Halima Mdee





Kutoka kushoto ni Halima Mdee, Ester Bulaya na Neema Hamid







Wakiwa mazoezini












Wakipewa Vyeti baada ya kuhitimu mafunzo hayo
Mbunge Ester Bulaya akipewa cheti na Rais Kikwete





Mbunge Zitto Kabwe akipokea cheti chake



Chama cha CHADEMA na Hali ya sintofahamu


CHADEMA ni Chama kikuu cha upinzani ukilinganisha na vyama vingine kwasasa. Miaka ya hivi karibuni kilijipatia sifa na umaarufu mkubwa miongoni mwa wananchi wanaopenda mabadiliko. Hali Inayoendelea kwa sasa ndani ya CHADEMA kwa kiasi fulani imewaacha wananchi wengi na hasa wafuasi wake na sintofahamu huku uchaguzi mkuu ukikaribia. Je nini kinaitafuna CHADEMA?







Violence is never a solution in politics. It aims at instilling fear in the people and cowing them to submit. I condemn in strongest possible terms the Criminal acts inflicted on Mr. Yona, CHADEMA Temeke chairperson. This cruelty is a cowardly act. Mr. Yona's sin is one- opposing unjust decisions by party central committee against some party leaders.
I challenge all CHADEMA leaders to renounce violence as an instrument of politics.




Mmmhhhh!!!????







Bundi Kaingia Chadema!


Wakili Tundu Lissu amenituhumu kuwa nimehongwa magari 2 na mheshimiwa Nimrod Mkono. Mimi ninamiliki gari moja mbili, freelnder ninayotumia Dar Es Salaam na Toyota Carina ninayotumia jimboni. Tuhuma hii haimo katika tuhuma nilizotuhumiwa nazo na kuandikiwa na chama ili kujibu. Kama Tundu lissu anadhani tuhuma hii ana ushahidi nayo wa kutosha aiongeze kwenye tuhuma walizoniandikia ili niweze kujitetea kwenye vikao, vinginevyo ni mipasho tu. Nawapa changamoto Tundu lissu na wenzake kama wana tuhuma Mpya dhidi yangu waniandikie kwa mujibu wa taratibu. Tuhuma nilizo nazo hivi sasa na ambazo nimezikatia rufaa katika Baraza Kuu zinahusu mkakati wa kugombea uenyekiti Taifa na kutaka mahesabu ya chama yakaguliwe na CAG.