Translate

Tangazo la Hadithi

Showing posts with label Vichekesho. Show all posts
Showing posts with label Vichekesho. Show all posts

Friday, 8 August 2014

CHEKA UNENEPE - Girlfriend na Boyfriend





Kijana mmoja alikuwa akichat kwenye simu na girlfriend wake na mazungumzo yao yalikuwa kama ifuatavyo:




Boyfriend: Baby unaweza kuja Home mara moja?


Girlfriend: Hapana, siwezi mpenzi, maana jana sikunyoosha nguo, hivyo nguo zangu zote zimekunjana na umeme umekatika.


Boyfriend: Aaah pole sana Baby... kwa hiyo hela uliyoniomba jana itakuwaje? maana nilitaka uje uchukue.


Girlfriend: Huooo! Yaani baby kama mchawi vile...nilipomaliza kusoma tu meseji yako na umeme nao umerudi...Nisubiri dakika tatu tu nakuja baby.


Chezea mademu wa siku hizi!!!











Monday, 31 March 2014

CHEKA UNENEPE - Mke na Mume









Bwana mmoja na mke wake mazungumzo yao yalikuwa kama ifuatavyo:

Mke: Je miaka 10 na mimi ni kama nini?

Mume: Ni kama sekunde.

Mke: Je dola 1000 kwa ajili yangu ni kama nini?

Mume: Ni kama senti.

Mke: OK, nipe basi senti.

Mume: Subiri kama sekunde hivi.









Sunday, 30 March 2014

CHEKA UNENEPE - Mzungu na Mchungaji













Mzungu alifiwa na mbwa wake akampeleka kanisani ili aombewe.

MCHUNGAJI akamkaripia kwa ukali na kumwambia hatuombei mbwa hapa!

Mzungu akauliza ni wapi wanaombea mbwa?  maana nina sadaka ya shilingi MILIONI 5 kwa MCHUNGAJI atakayemuombea mbwa wangu!

MCHUNGAJI akajibu, aaah! Mbona hukusema mapema kuwa mbwa wako ni mkristo?

Haya mlete nimuombee! 


Duuuuh, Pesa Bwana!!!









Tuesday, 21 January 2014

CHEKA UNENEPE - Baba na Kijana wake











Baba: Nataka umuoe msichana nitakayekuchagulia.


Kijana: Hapana baba, ninaye ninayempenda.


Baba: msichana mwenyewe niliyekuchagulia ni mtoto wa Bill Gates.


Kijana: Kama hivyo sawa.



Baba akaenda kwa Bill Gates.


Baba: Nataka binti yako aolewe na kijana wangu.


Bill Gates: Hapana!


Baba: Kijana wangu ni mkurugenzi wa Benki ya Dunia.


Bill Gates: Kama hivyo sawa.



Baba akaenda kwa rais wa benki ya dunia.


Baba: Mchague mwanangu kuwa mkurugenzi


Rais wa Benki ya Dunia: Hapana.


Baba: Ni mkwe wa Bill Gates.


Rais wa Benki ya Dunia: Kama hivyo sawa












CHEKA UNENEPE - Mgombea Urais na Waandishi wa Habari











Jamaa mmoja ambaye alikuwa anataka kugobea nafasi ya urais chini mwake alikutana na waandishi mbalimbali kwa ajili ya kumuuliza mgombea huyo maswali. Mwandishi mmoja alianza kumuuliza swali na mazungumzo yao yalikuwa kama ifuatavyo.


Mwandishi: Muheshimiwa mgombea urais je unafikiri ni mambo gani ambayo utaweza kuifanyia nchi hii kama utashinda nafasi ya urais?


Mgombea urais: Nafikiri kitu cha kwanza nitakachofanya nikipata urais nitahakikisha natimiza ndoto yangu ya kuiwezesha nchi yangu kuwa ndio nchi ya kwanza kufika kwenye jua.


Mwandishi: Lakini muheshimiwa kwenye jua kuna joto kali sana sasa itakuwaje? si tutawapoteza hao wana sayansi utakaowatuma kwenda huko kwenye jua?


Mgombea urais: Ha ha ha haaaa Bwana mwandishi, unafikiri mimi ni mjinga? tutawatuma kwenda huko usiku  sio mchana.



Duuuuuh!!!!!!!!










Tuesday, 7 January 2014

CHEKA UNENEPE - Juma kwenye sherehe ya wanyakyusa






Jamaa mmoja aitwaye JUMA alivamia sherehe ya harusi ya Wanyakyusa na kujifanya na yeye ni mwanafamilia wa bwana harusi. Wakati wa utambulisho wa ndugu wa bwana harusi wakaanza kusimama mmoja mmoja na kutaja jina lake.

Wa kwanza akasema: Naitwa Mwakalebela.

Wa pili akasema: Naitwa Mwasikili

Wa tatu akasema: Naitwa Mwakipesile 

Wa nne akasema: Naitwa Mwakasungura

Wa tano akasema: Naitwa Mwambela

Wa sita akasema: Naitwa Mwakatundu

Ilipofika zamu ya Juma akafikiria kisha akadhani kuwa kila jina katika kabila lile ni lazima uanze na "MWA", basi akainuka kwa makonfidensi na kupaza sauti "Naitwa MWAJUMA"








Sunday, 5 January 2014

CHEKA UNENEPE - Fundi wa gari na Mteja wake







Jamaa mmoja alipeleka gari yake gereji ili ipakwe rangi. Mazungumzo yake na Fundi yalikuwa kama ifuatavyo.

Jamaa: Fundi paka rangi gari yangu isipokuwa rangi nyekundu, kijivu na aina yoyote ile. Je nije kuichukua lini?

Fundi: Njoo siku yoyote isipokuwa jumatatu hadi jumapili.









Saturday, 4 January 2014

CHEKA UNENEPE - Mbegu









Jamaa watatu toka kijijini walikwenda mjini kumtembelea ndugu yao. Walipofika wakakaribishwa soda wakanywa. Walipoondoka wakati wapo njiani mmoja akamnong'oneza mwenzie huku akimuonyesha kisoda cha soda aliyokunywa, " mwenzio nimeondoka na mbegu, wewe je?"