Translate

Tangazo la Hadithi

Showing posts with label Cheka unenepe. Show all posts
Showing posts with label Cheka unenepe. Show all posts

Friday, 8 August 2014

CHEKA UNENEPE - Girlfriend na Boyfriend





Kijana mmoja alikuwa akichat kwenye simu na girlfriend wake na mazungumzo yao yalikuwa kama ifuatavyo:




Boyfriend: Baby unaweza kuja Home mara moja?


Girlfriend: Hapana, siwezi mpenzi, maana jana sikunyoosha nguo, hivyo nguo zangu zote zimekunjana na umeme umekatika.


Boyfriend: Aaah pole sana Baby... kwa hiyo hela uliyoniomba jana itakuwaje? maana nilitaka uje uchukue.


Girlfriend: Huooo! Yaani baby kama mchawi vile...nilipomaliza kusoma tu meseji yako na umeme nao umerudi...Nisubiri dakika tatu tu nakuja baby.


Chezea mademu wa siku hizi!!!











Monday, 31 March 2014

CHEKA UNENEPE - Mke na Mume









Bwana mmoja na mke wake mazungumzo yao yalikuwa kama ifuatavyo:

Mke: Je miaka 10 na mimi ni kama nini?

Mume: Ni kama sekunde.

Mke: Je dola 1000 kwa ajili yangu ni kama nini?

Mume: Ni kama senti.

Mke: OK, nipe basi senti.

Mume: Subiri kama sekunde hivi.









Sunday, 30 March 2014

CHEKA UNENEPE - Mzungu na Mchungaji













Mzungu alifiwa na mbwa wake akampeleka kanisani ili aombewe.

MCHUNGAJI akamkaripia kwa ukali na kumwambia hatuombei mbwa hapa!

Mzungu akauliza ni wapi wanaombea mbwa?  maana nina sadaka ya shilingi MILIONI 5 kwa MCHUNGAJI atakayemuombea mbwa wangu!

MCHUNGAJI akajibu, aaah! Mbona hukusema mapema kuwa mbwa wako ni mkristo?

Haya mlete nimuombee! 


Duuuuh, Pesa Bwana!!!









Tuesday, 7 January 2014

CHEKA UNENEPE - Juma kwenye sherehe ya wanyakyusa






Jamaa mmoja aitwaye JUMA alivamia sherehe ya harusi ya Wanyakyusa na kujifanya na yeye ni mwanafamilia wa bwana harusi. Wakati wa utambulisho wa ndugu wa bwana harusi wakaanza kusimama mmoja mmoja na kutaja jina lake.

Wa kwanza akasema: Naitwa Mwakalebela.

Wa pili akasema: Naitwa Mwasikili

Wa tatu akasema: Naitwa Mwakipesile 

Wa nne akasema: Naitwa Mwakasungura

Wa tano akasema: Naitwa Mwambela

Wa sita akasema: Naitwa Mwakatundu

Ilipofika zamu ya Juma akafikiria kisha akadhani kuwa kila jina katika kabila lile ni lazima uanze na "MWA", basi akainuka kwa makonfidensi na kupaza sauti "Naitwa MWAJUMA"