Translate

Tangazo la Hadithi

Friday, 23 August 2013

KACHIKI - SEHEMU YA 3


BABA YAKE KACHIKI MZEE NYARONGO AFIKA SHULENI.





Mwalimu mkuu alimpa Kachiki Barua ili akampe baba yake mzee Nyarongo. Alipofika nyumbani alimkuta baba yake amesharudi kutoka kazini kwake anakofanya kazi ya useremala, hivyo alimkabidhi ile barua aliyopewa na mwalimu mkuu ili ampe baba yake. Alivyomkabidhi baba yake barua mama yake wa kambo alianza kumwambia baba yake Kachiki kuwa alishamueleza huyu mtoto yani Kachiki ni mkorofi na msumbufu sana, hivyo ana uhakika kabisa amefanya kosa kubwa sana na ndiyo maana walimu wameshindwa kuvumilia na safari hii wameamua kumuita aende shuleni. Inavyoonekana tayari walimu wameshachoka na vituko vyake. Baba yake Kachiki alishikwa na hasira sana na kumwambia Kachiki kuwa kama amefanya upuuzi wowote huko shuleni atamtambua. Siku hiyo Kachiki alikosa raha kabisa kwani hata yeye hakujua kwanini baba yake aliitwa shuleni. Usiku hakuweza hata kupata usingizi alikuwa akisali na kuomba Mungu amsaidie na kusiwe na tatizo kubwa aliloitiwa baba yake huko shuleni.


Asubuhi alivyoamka Kachiki aliendelea na ratiba zake za kila siku halafu akaenda shuleni. Alivyorudi kutoka shule alimkuta baba yake amesimama kwenye  mlango wa mbele wa nyumba yao, akiwa na ghadhabu huku akiwa ameshika fimbo kubwa mkononi. Mama yake wa kambo alikuwa amekaa kwenye mkeka akiwa mwenye ghadhabu pia. Kachiki hakujua kinachoendelea, alivyowakaribia aliwasalimia lakini badala ya kujibu mama yake wa kambo alianza kumgombeza kwa sauti ya juu, na baba yake hakumpa hata nafasi ya kujua nini kinachoendelea, badala yake alimshika kwa nguvu na kuanza kumpiga, alimpiga kichwani, mgongoni na sehemu zote za mwili. Wakati akimpiga hivyo mama yake wa kambo alikuwa akishirikiana naye kwa kumpa kipigo Kachiki. Maskini Kachiki hakukumbuka chochote, alichosikia kwa mara ya mwisho yalikuwa ni maneno ambayo baba yake mzee Nyarongo aliyosema “Kwanini umeitia aibu hii familia” halafu akazimia.

No comments:

Post a Comment