WALIMU WANAJARIBU
KUMSAIDIA KACHIKI
Ingawa
Kachiki alikuwa na akili sana darasani alianza kushuka kwenye mitihani yake
kwasababu ya matatizo aliyokuwa anayapitia. Mwanzoni alikuwa nakuwa wa kwanza
darasani lakini alianza kushuka mpaka kufikia kushika nafasi ya kumi na tano
kutoka mwisho kwenye darasa la wanafunzi zaidi ya hamsini.
Mwanzoni
alivyokuwa anakuwa wa kwanza darasani mama yake wa kambo mama Selina alikuwa
akisema kuwa anakuwa wa kwanza kwasababu anaibia kwenye mitihani, na Kachiki
alipo jitahidi kujitetea mama Selina alikuja juu na kumwambia baba yake kuwa
Kachiki hamuheshimu ndiyo maana anafikia hatua ya kujibizana naye. Maskini
Kachiki badala ya kupongezwa kwa kufaulu akawa anaishia kuadhibiwa vikali na
baba yake kwa kuchapwa viboko visivyo na idadi.
Na
alivyoanza kushuka darasani mama yake wa kambo mama Selina aliishia kufurahia
na kumwambia baba yake na Kachiki kuwa mwanae alikuwa anagelezea kwenye
mitihani ndio maana alikuwa anafaulu na sasa anafeli kwasababu walimu wamekuwa
wakali mno na wameweka sheria kali sana kwa yeyote atakayeibia kwenye mitihani.
Siku
moja mwalimu wa darasa wa Kachiki aliyekuwa anaitwa mwalimu Songambele alimwita
Kachiki na kuanza kumuuliza kwanini siku zote amekuwa akichelewa kufika shuleni
na pia kwanini ameanza kushuka kwenye masomo yake darasani. Pia hata akipewa kazi za shule na mazoezi ya
kwenda kufanya nyumbani amekuwa hafanyi kabisa au amekuwa hamalizi. Kachiki
alianza kulia na kushindwa kujibu chochote. Mwalimu Songambele ndipo alianza
kuhisi kuwa kuna kitu kinachoendelea katika maisha ya mwanafunzi wake Kachiki.
Hivyo mwalimu Songambele akamuacha kwanza atulie kidogo na kunyamaza kulia ili
aweze kumuuliza vizuri zaidi. Kipindi hicho Kachiki alikuwa bado ni binti mdogo
akisoma darasa la nne.
Kachiki alivyonyamaza kulia na kutulia kidogo mwalimu wake Songambele alianza kumuuliza tena, basi Kachiki alianza kumueleza kuhusu maisha yake anayoishi huko nyumbani na ratiba yake ilivyo ngumu kuanzia asubuhi anavyoamka mpaka jioni anavyorudi nyumbani kutoka shuleni na usiku anavyokwenda kulala. Na jinsi ambavyo anakosa hata muda wa kujisomea na kufanya mazoezi anayopewa shuleni. Kachiki akaendelea kumueleza mwalimu wake kuwa akifika shuleni ndio anaona sehemu yake ya kupumzikia na kupata usingizi japo kidogo. Ndio maana amekuwa mtu wa kusinzia darasani kwasababu anakuwa amechoka sana na anakuwa na usingizi mzito mno. Akiwa mlezi wa wanafunzi na pia mzazi wa watoto wake wawili wadogo mwalimu Songambele alipatwa na uchungu mno tena sana. Akapiga picha watoto wake hao wadogo ndio wawe wanaishi maisha haya! Huruma ikamjia sana. Akafikiri na kuona kuwa hata kama labda Kachiki hasemi ukweli na labda mama yake wa kambo anamfundisha tu kazi akiwa ni mtoto wa kike lakini kwa kumuangalia tu Kachiki utagundua kuwa huyu binti ana matatizo ya kifamilia na pia hana mtu wa kumuangalia na kumuongoza. Maana Kachiki alikuwa mchafu sana. Sketi yake ilikuwa imepauka na imetoboka toboka sana. Alikuwa hana viatu hivyo alikuwa akienda shuleni pekupeku. Hilo mwalimu halikumshangaza sana kwani ni wanafunzi wachache sana walikuwa wanavaa viatu shuleni hapo, wengi walikuwa wanavaa kandambili na wengine walikuwa hawana kabisa hata kandambili, lakini bado walionekana wasafi kidogo kuliko Kachiki maana hata wale wenye sare za shule zilizochakaa walikuwa wasafi kuonyesha kuwa sare zao zilikuwa zikifuliwa angalau mara kadhaa kwa wiki. Kwa karibu Kachiki alikuwa akinuka na kutoa harufu. Hata ngozi yake nzuri ya rangi ya chungwa ilikuwa imesinyaa kuonyesha kuwa hata kupata chakula kwake ni shida, ingawa uzuri wake wa sura bado ulikuwa ukionekana. Mwalimu Songambele akamuuliza Kachiki kama yeye ndio anafua nguo za watu wote pale nyumbani kwanini basi anashindwa kufua nguo zake mpaka anakuwa mchafu kiasi kile na kufikia hatua ya kutoa harufu? Kachiki akamjibu mwalimu wake wa darasa ya kuwa mama yake wa kambo mama Selina amekuwa akimwambia kuwa wakati akifua nguo zao asifue nguo zake na pia asichanganye na nguo zake kwani atawaambukiza chawa pia hamna sabuni ya kufulia nguo zake. Na pia mara nyingi akimkuta anafua nguo zake huwa anamuuliza amepata wapi sabuni na huo muda wa kupoteza mpaka kuweza kufua matambara yake badala ya kufanya kazi za pale nyumbani. Kachiki alimweleza mwalimu wake mambo mengi mno ambayo hamna mtu yeyote mwingine anayejua ingawa hata majirani walikuwa wanaona na kufahamu jinsi Kachiki alivyokuwa akiteseka lakini hawakufahamu mambo mengi ambayo Kachiki alimueleza mwalimu wake wa darasa, mwalimu Songambele.

Baada
ya kusikia kuhusu maisha ya Kachiki anayoishi huko nyumbani mwalimu wa darasa
akaona amshirikishe pia na mwalimu mkuu ili waone jinsi watakavyomsaidia
Kachiki maana aliona hili tatizo ni kubwa sana tofauti na alivyofikiria.
Akajiona yeye na walimu wenzake ni wenye makosa mno tena sana kwa kumuadhibu
Kachiki kila siku kwa sababu za uchelewaji, kutohudhuria shuleni bila sababu
maalum, kuja shuleni akiwa mchafu, kutofanya homework, kusinzia darasani n.k.
Kama kwa siku hiyo tu amechapwa viboko karibia 15 na walimu tofauti kwa makosa
tofauti na mpaka kuwa ndio mazungumzo ya walimu kwa siku hiyo ofisini kwao. Alianza
mwalimu wake wa Hisabati kusema kwamba kuna mwanafunzi anaitwa Kachiki lakini akimpa homework hafanyi na kila siku lazima amchape hata leo amemtandika sana,
akadakia mwalimu wa sayansi kwa kusema kuwa yule binti ana akili lakini ni
mvivu mno tena sana kama leo kaishia kumchapa viboko vya kutosha kwani aliwapa
homework hajafanya pia anaishia tu kulala darasani. Akadakia mwalimu wa
kingereza kwa kusema kuwa tena sijui somo lake halipendi maana kila siku yeye ana vipindi
vya asubuhi viwili lakini huyo Kachiki haudhurii ama anakuja wakati kipindi
kinakaribia kuisha kama leo kaingia dakika 20 kabla ya kipindi kuisha akamfukuza nje na kumwambia apige magoti juani mpaka hizo dakika 20
zitakavyoisha akitoka ndio aingie. Mwalimu wa zamu naye akadakia kama kawaida
leo kamchapa viboko sita kwa kuchelewa kufika shule ingawa ni mpole lakini
atakuwa na kiburi mototo gani asiyesikia kila siku anaadhibiwa lakini anarudia
makosa hayo hayo. Hayo ndio mazungumzo waliyokuwa wakiyaongea walimu ofisini
kwao kwa siku hiyo ambayo yakamfanya mwalimu wa darasa aamue kumuita Kachiki
ili kuongea naye. Akiwa mwalimu wa darasa hata yeye mwalimu Songambele amekuwa
akimuadhibu sana Kachiki kwa kudhani kuwa labda ni mvivu hivyo kwa kuadhibiwa
atajirekebisha, baada ya kumsikiliza Kachiki akajikuta akinyong’onyea na kujilaumu
kwa kiasi fulani kushindwa kulitambua hilo mapema.
Hivyo
baada ya mashauriano ya hapa na pale mwalimu mkuu na mwalimu wa darasa waliamua
kumuita mzazi wa Kachiki, baba yake mzee Nyarongo kufika shuleni kwasababu
walifikiri ya kuwa itakuwa baba yake hafahamu kinachomtokea binti yake
nyumbani. Maana imekuwa ni tabia ya mama wengi wa kambo kuwa wanafiki na
kuonyesha upendo kwa watoto wao wa kambo pindi baba zao wawapo nyumbani lakini
wakiondoka tu ndio mama wa kambo wanapobadilika na mateso kwa watoto hao kuanza.
No comments:
Post a Comment