Translate

Tangazo la Hadithi

Tuesday, 4 February 2014

Wanafunzi wa St. Anne Marie wafanya uharibifu shuleni kwao



Wanafunzi wa St. Anne Marie iliyoko Mbezi jijini Dar wafanya uharibifu mkubwa wa mali na majengo ya shule yao. Wanafunzi hao wamefanya uharibifu mkubwa katika chumba cha computer ambapo computer zipatazo 40 za mezani zimeharibiwa na laptop 16 hazijulikani zilipo.

Wanafunzi hao walivamia maeneo mbalimbali ya shule hiyo alfajiri ya kuamkia tarehe 3 mwezi wa kwanza mwaka 2014 majira ya saa nane usiku na kufanya uharibifu huo. Wanafunzi hao wamevunja pia vioo vya majengo na magari. Mabasi ya shule na magari mengine yapatayo 17 yamevunjwa vioo na kuharibiwa vibaya.





Chumba cha Computer katika shule ya St. Anne Marie kinavyoonekana baada ya uharibifu uliofanywa na wanafunzi






Chumba cha Computer katika shule ya St. Anne Marie kinavyoonekana baada ya uharibifu uliofanywa na wanafunzi






Mabasi ya shule yakiwa yameharibiwa vibaya






Mkuu wa wilaya Jordan Rugimbana akiangalia chumba cha computer kilichofanyiwa uharibifu






Mkuu wa wilaya ya Kinondoni, Jordan Rugimbana (kushoto) akiwa pamoja na Kamanda wa Polisi wa mkoa wa kipolisi wa Kinondoni, Camilius Wambura wakikagua uharibifu uliofanywa na wanafunzi wa shule  sekondari ya St. Anne Marie iliyopo Mbezi jijini Dar es salaam.




No comments:

Post a Comment